OSWAMS yawa muarobaini wa maji taka nchini

Kampuni ya On site Sustanable Waste Water Management Systems(OSWAMS) imekuja na muarobaini wa kero ya maji taka iliyokuwa sugu katika  makazi ya watu  pamoja na taasisi mbalimbali hapa nchini.

Haya yamebainishwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya OSWAMS Bw.Juma .Nassor wakati wa ziara ya wageni kutoka wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii walipotembelea moja ya mradi wa kota za Polisi Mikocheni jijini Dar es salaam ambapo kampuni hiyo imejenga mfumo wa kudhibiti  ya maji taka.

Katika ziara hiyo Bw. Juma Nassor amesema kampuni ya OSWAMS imekuja na mfumo maalumu na wa kisasa ambao kazi yake ni kubadilisha maji taka yanayotoka katika chemba ya choo, bafuni pamoja na jikoni ili yaweze kutumika katika matumizi mengine ikiwemo umwagiliaji na ujenzi.

Amesema mfumo wa OSWAMS una faida nyingi katika makazi moja ikiwa ni kuondoa gharama za kunyonya maji taka mara kwa mara katika makazi,kuondoa harufu ambayo ni kero katika jamii, na pia  mfumo  huo  unasaidia kuyafanya maji taka yatumike katika matumizi mengine.

Akitoa ushuhuda wa jinsi mfumo unavyofanyaka kazi Mwalimu wa Mazingira katika shule ya Liberman ya Mikocheni jijini hapa Brenda Magai amesema kabla ya kujenga mfumo wa OSWAMS shule hiyo ilikuwa ikinyonya maji mara mbili kwa mwezi.

Aidha,amesema tangu OSWAM wajenge mfumo wao hawajawahi kunyonya maji tangu mwaka 2015 hadi mwaka 2017, hivyo kupelekea kuokoa fedha nyingi zilizokuwa zimetengwa ili kunyonya maji taka.

Share

Subscribe to our Newsletter!

Sign up to receive environmental news and updates!

dev
Notice: ob_end_flush(): failed to send buffer of zlib output compression (0) in /home4/oswams/public_html/wp-includes/functions.php on line 3783